Dk.Hussein Ali Mwinyi ameondoka nchini leo kuelekea Maputo nchini Msumbiji

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameondoka nchini leo kuelekea Maputo nchini Msumbiji kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa dharura wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), utakaofanyika nchini humo Mei 27,2021.

Akiondoka katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Abeid Karume Zanzibar, Rais Dk. Mwinyi aliagwa na Viongozi mbali mbali wa Serikali wakiongozwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdallah pamoja na viongozi wengine.

Mkutano huo wa nchi za (SADC) unaofanyika nchini Msumbuji unatarajia kujadili masuala ya hali ya ulinzi na usalama unawajumuisha viongozi wakuu kutoka nchi za Jumuiya (SADC) zikiwemo Msumbiji, Malawi, Tanzania, Botswana, Afrika Kusini,  na Zimbwabwe.

Rais Dk. Mwinyi anatarajia kurejea nchini Alkhamis ya Mei 27 mwaka huu.